Wafanyakazi wakataa nyongeza ya mishahara

Mgomo wa wafanyakazi nchini Afrika Kusini
Image caption Mgomo wa wafanyakazi nchini Afrika Kusini

Mgomo wa wiki tatu wa wafanyakazi wa Umma nchini Afrika Kusini, sasa utaendelea kwa muda usiojulikana, baada ya Chama cha muungano wa vyama vya wafanyakazi nchini humo COSATU, kukataa nyongeza ya asilimia 7.5 iliyotolewa na serikali.

Katibu mkuu wa COSATU, Zwelinzima Vavi, amesema viongozi wengi wa vyama vya wafanyakazi ambao ni wanachama wake walipiga kura kukata nyogesa hiyo iliyotolewa na serikali.

Hata hivyo COSATU inasema vyama vingine vidogo vidogo vimetofautiana kuhusu nyingesa hiyo.

Mazungumzo zaidi ya kujaribu, kumaliza mgomo huo yanatarajiwa kuanza upya baadaye hii leo.

Serikali ya Afrika Kusini imetoa nyongesa ya asilimia 7.5 lakini wafanyakazi hao wanataka nyongesa ya asilimia 8.6.