Uchaguzi wa urais wanukia Guinea

Waziri Mkuu wa Guinea
Image caption Waziri Mkuu wa Guinea

Wiki chache tu kabla ya kufanyika kwa duru ya pili ya uchaguzi wa urais nchini Guinea, Waziri Mkuu wa nchi hiyo, ametoa pendekezo kwa utawala wa kijeshi nchini humo kuipa wizara ya mambo ya ndani madaraka zaidi ili kusimamia uchaguzi huo.

Waziri Mkuu Jean-Marie Dore amependekeza kuwa kiongozi wa kijeshi nchini humo Generali Conate, aagize wizara hiyo kusimamia zoezi hilo kwa ushirikiano na tume huru ya uchaguzi.

Lakini mmoja wa wawaniaji wa kiti hicho cha urais, Cellou Dalein Dellou, amesema pendekezo hilo litamsaidia mpinzani wake Alpha Conde.

Waandishi wa Habari wanasema duru hiyo ya pili ya uchaguzi wa urais ambao utahusisha watu wawili kutoka kabila tofauti, huenda ukazua hali ya wasi wasi.