Ripoti kuhusu Rwanda kutolewa Octoba-UN

Rais wa Rwanda
Image caption Rais wa Rwanda

Afisa mkuu wa Umoja wa Mataifa, anayeshughulika na masuala ya haki za kibinadam, amesema, atachelewesha kutolewa kwa ripoti iliyogadhabisha serikali ya Rwanda.

Ripoti hiyo ilidai wanajeshi wa Rwanda walihusika na mauaji ya kimbari katika Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo, hatua ambayo iliifanya serikali ya Rwanda kutishia kuwaondoa wanajeshi wake wa kutunza amani kutoka kwa kikosi cha Umoja wa mataifa.

Kamishna mkuu wa shirika la kutetea haki za kibindam wa Umoja huo Navi Pillay, amesema ripoti hiyo itatolewa mwezi ujao na itajumuisha ripoti rasmi kutoka kwa serikali Rwanda.

Ripoti hiyo imenakili habari kuhusu kesi mia sita za ukiukwaji wa haki za kibinadamu Mashariki mwa Congo kati ya mwaka wa 1993 na 2003.