Houllier kocha mpya Aston Villa

Gerard Houllier
Image caption Gerard Houllier

Meneja wa zamani wa Liverpool na Lyon Gerard Houllier, ameteuliwa kuwa meneja mpya wa Aston Villa.

Houllier mwenye umri wa miaka 63 ameacha kazi yake ya kuwa Mkurugenzi wa Ufundi katika Shirikisho la Soka la Ufaransa na kurejea katika soka ya England baada ya kuwa nje kwa miaka sita.

Anachukua nafasi ya meneja wa muda Kevin MacDonald, aliyeiongoza Aston Villa tangu Martin O'Neill alipoondoka tarehe 9 mwezi wa Aprili.

Mtendaji Mkuu wa Aston Villa Paul Faulkner amesema: "Houllier anaelewa maadili na thamani ya klabu yetu".

Msaidizi wa Houllier wakati akiwa Liverpool, Phil Thomson, ametajwa huenda akamsaidia meneja huyo katika klabu ya Aston Villa, lakini hata hivyo Thomson ameamua kuendelea na kazi yake ya uchambuzi wa soka katika televisheni.

Haijafahamika Houllie mkataba wake katika klabu hiyo ni wa muda gani.