Sudan Kusini 'bomu linalosubiri kulipuka'

Image caption Sudan

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani alisema, kura ya maoni juu ya uhuru wa Sudan Kusini ni " bomu linalosubiri kulipuka."

Kura hiyo inatarajiwa kupigwa mwezi Januari na Bi Clinton amesema matokeo hayo "hayaepukiki"- wakitaka kujitenga.

Alitoa wito kwa viongozi wa Sudan na wa kimataifa kufanya zaidi katika kujiandaa kwa ajili ya uchaguzi.

Kura ya maoni ilikuwa ni sehemu ya makubaliano ya amani ya mwaka 2005 kwa ajili ya kumaliza miongo miwili ya mapigano baina ya upande wa kaskazini na kusini wenye utajiri wa mafuta.

Bi Clinton alisema hatarajii kuwa upande wa kaskazini utaridhishwa kupoteza mapato yake ya mafuta kutoka kusini lakini viongozi wa kusini lazima "uwape nafasi" na kaskazini "labda kama watataka miaka mengine ya vita."

Sudan Kusini, ambapo wengi wao ni Wakristo au hufuata dini za kimila, tayari inajitawala kwa kiasi fulani na inaongozwa na waliokuwa waasi wa kundi la SPLA, waliopigana na wengi walio waislamu, na waarabu wa kaskazini mpaka yalipofanyika makubaliano mwaka 2005.

Balozi wa Umoja wa Mataifa wa Rais Barack Obama, Susan Rice, alitangaza kuwa Bw Obama anatarajiwa kuhudhuria mkutano maalum unaohusu maisha ya usoni ya Sudan Septemba 24.

Alisema Bw Obama anauona mkutano huo "kuwa muhimu sana kwa kuvutia jumuiya za kimataifa" katika kura ya maoni kabla ya "siku 100 za mwisho kabla ya kura hiyo."

Kumekuwa na onyo zikitolewa kuwa eneo hilo, ambalo ni miongoni mwa nchi maskini duniani, haliko tayari kupiga kura ya maoni.

Uandikishwaji wa wapiga kura haujaanza, na swali la kwamba nani hasa ataruhusiwa kupiga kura haijaamuliwa.

Mwezi uliopita Sudan Kusini ilianzisha mashindano ya kutunga wimbo mpya wa taifa kwa ajili ya eneo hilo.