Wanajeshi wa Ubeljiji washtakiwa kwa mauaji

Ramani ya Rwanda

Wanajeshi watatu wa nchi ya Ubelgiji, wamefunguliwa mashtaka mjini Brussels kwa tuhuma za kuhusika na mauaji ya kimbari nchini Rwanda, mwaka wa tisini na nne.

Kesi hiyo imewasilishwa mahakamani na waathiriwa wa mauaji hayo ya kimbari wanaoishi Ubelgiji.

Wanadai wanajeshi hao watatu wa Ubelgiji, waliokuwa miongoni mwa wanajeshi wa umoja wa mataifa wa kulinda amani, walihusika kwa njia moja au nyingine kwenye mauaji hayo.

Wanadai wanajeshi hao hawakuwasaidia licha ya kwamba walikuwa wametafuta hifadhi kwenye shule moja ambapo wanajeshi hao walikuwa walikuwepo.

Nchini Rwanda kwenyewe, vuguvugu linalotetea haki za waathirika wa mauaji hayo ya Kimbari, lijulikanalo kama IBUKA, limeunga mkono kufunguliwa kwa kesi hiyo, dhidi ya wanajeshi hao wa Ubelgiji.

Ubeljiji iliyaondoa wanajeshi wake nchini Rwanda bada ya majeshi kadhaa kuawa na makundi yaliyokuwa yakitekeleza mauaji ya kimbari mwaka 1994.