LRA yashambuliwa na waasi Darfur

Joseph Kony

Kundi la waasi wa Darfur huko Sudan limesema kwamba limeshambulia kundi asi la Uganda la Lord's Resistance Army.

Mwanachama wa juu wa kundi la Liberation and Justice amesema kwamba LRA walishambulia ngome yao kusini mwa Darfur hapo jumatano.

Taarifa ya awali ilidai kwamba kamanda mmoja wa LRA alikuwa amevuka Sudan Kusini bila wapiganaji wake wapatao 30.

Maafisa Sudan Kusini wamedai kwamba utawala wa Khartoum anafadhili kundi la LRA kutekeleza mashambulio eneo la kusini ili kuivuruga shughuli ya kura ya maoni mapema mwakani.

Hata hivyo Khartou imekanusha madai hayo.

Katika miezi ya karibuni waasi wa LRA wametuhumiwa kushambulia maeneo ya Sudan Kusini na kupelekea mamia ya wakaazi kukimbia makwao. Kundi hilo limedaiwa kuendesha harakati zake katika nchi tatu ikiwa ni pamoja na Jamuhuri ya Afrika ya Kati, Mashariki mwa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo pamoja na Sudan Kusini.

Harakati za jeshi la Uganda ikisaidiwa na wanajeshi wa Congo kuzima shughuli za LRA nchini Congo hazijafanikiwa kwani waasi hao wameendelea kushambulia vijiji DRC na Sudan Kusini.