Ufaransa kuchunguza kifo cha Habyarimana

Kundi la majaji wa Ufaransa na wataalam wa sheria leo linatarajiwa kuanza uchunguzi utakaodumu kwa wiki moja nchini Rwanda wa mauaji ya Rais Juvenal Habyarimana miaka kumi na sita iliyopita.

Ndege iliyombeba Bw Habyarimana ilidunguliwa na kombora tarehe sita mwezi April mwaka wa 1994 na kuchochea mauaji ya kimbari nchini Rwanda .

Image caption Habyarimana na mkewe

Majaji hao wanatumia fursa ya uhusiano ulioanza kuimarika kati ya nchi hizo mbili.

Uchunguzi wa awali wa Ufaransa juu ya mauaji ya Habyarimana ulisababisha Rwanda kuvunja uhusiano na Ufaransa mwaka wa 2006.