England yapanda kiwango cha soka FIFA

Wachezaji wa England
Image caption Wachezaji wa England wakishangilia bao

Ushindi mara mbili mfululizo katika mechi zake mbili za ufunguzi wa kufuzu mashindano ya Euro 2012, yamesababisha England kusogea nafasi moja juu katika viwango vya FIFA vya ubora wa soka na sasa inashikilia nafasi ya sita.

Hispania bado imeendelea kung'ang'ania kileleni, ikifuatiwa na Uholanzi, Ujerumani nafasi ya tatu, Brazil ya nne na Argentina ipo nafasi ya tano.

Jamhuri ya Ireland nayo imepanda nafasi tatu hadi kufikia nafasi ya 33, Ireland ya Kaskazini imepiga hatua 14 hadi nafasi ya 45, Scotland nafasi ya 47 na Wales wapo nafasi ya 84.

Ufaransa kutokana na soka mbovu iliyoonesha siku za karibuni imeporomoka kwa mara ya kwanza na kufikia nafasi ya 27.

Kufuatia matatizo makubwa ya timu ya Ufaransa wakati wa Kombe la Dunia nchini Afrika Kusini, Ufaransa, ikiwa chini ya mwalimu mpya Laurent Blanc ilipoteza nyumbani mchezo wake wa ufunguzi wa kufuzu mashindano ya Euro 2012, walipofungwa bao 1-0 na Belarus, ingawa walijipapatua na kuwalaza Bosnia.

England pia haikufanya vizuri katika fainali za Kombe la Dunia nchini Afrika Kusini, lakini matokeo ya Euro 2010 yamewapandisha juu.

Vijana hao wa Fabio Capello waliwafunga Bulgaria mabao 4-0 na wakawalaza Uswiss mabao 3-1.

FIFA huwa wanatoa viwango vya ubora wa soka kwa nchi kwa mzunguko wa miaka minne, wakitumia michezo 159 ya kimataifa iliyochezwa ndani ya wiki tano.

Mashindano ya kufuzu kucheza Euro 2012 na ya Kombe la Mataifa ya Afrika 2012 ndio yenye pointi nyingi.

Zifuatazo ni timu kumi bora kwa ubora wa viwango duniani:

1.Spain

2. Netherlands

3. Germany

4. Brazil

5. Argentina

6. England

7. Uruguay

8. Portugal

9. Egypt

10. Chile