Guinea: wagombea wakuu kuelezea ghasia

Image caption wanajeshi walinda amani Guinea

Serikali ya Guinea imewaita wagombea wote wawili, aliyekuwa waziri mkuu Cellou Dalein Diallo na mwanasiasa mkongwe ambaye ni kiongozi wa upinzani Alpha Conde- ili waeleze kuhusu ghasia ambazo zimeongezeka wakati wa wikendi.

Waziri wa mawasiliano Talide Dialo ametangaza kupitia televisheni ya kitaifa kuwa mikutano ya kisiasa na kampeni zote zimesitishwa kwa sababu ya ghasia hizo.

Vurugu zilizotokea katika mji mkuu Conakry baada ya mahakama moja mjini humo kuwahukumu kifungo maafisa wawili wa tume ya uchaguzi ambao walikuwa wamepatikana na hatia ya wizi wa kura katika raundi ya kwanza ya uchaguzi iliyofanyika mwezi juni.