Afrika Kusini yajikongoja ubora wa soka

Wachezaji wa Bafana Bafana
Image caption Bafana Bafana

Afrika Kusini imeweza kupanda kiwango cha FIFA cha ubora wa soka duniani na kufikia nafasi ya 58.

Hii inafuatia ushindi iliyopata dhidi ya Ghana katika mchezo wa kirafiki na baada ya kuifunga Niger kwenye mchezo wa kufuzu kwa Kombe la Mataifa ya Afrika.

Hiyo ni nafasi bora kwa Bafana Nafana tangu mwaka 2007 na kwa bara la Afrika imepanda na kuwemo katika nchi kumi bora.

Kweingineko, Misri inayoshikilia nafasi ya juu Afrika, bado imo katika nchi bora kumi duniani kwa usakataji wa kandanda, wakati Ghana waliofika hatua ya robo fainali katika Kombe la Dunia, wamepanda nafasi tatu na kushika nafasi ya 20 duniani na kwa Afrika ipo nafasi ya pili.

Cape Verde iliyofanikiwa kuifunga Mali katika mchezo wa kufuzu kwa Kombe la Mataifa ya Afrika imesogea hadi nafasi ya 31 barani Afrika na duniani ipo nafasi ya 77.

Nchi bora kumi kwa soka barani Africa:

1. Misri (duniani nafasi ya 9)

2. Ghana (duniani nafasi ya 20)

3. Ivory Coast (duniani nafasi ya 23)

4. Gabon (duniani nafasi ya 31)

5. Nigeria (duniani nafasi ya 34)

6. Algeria (duniani nafasi ya 35)

7. Cameroon (duniani nafasi ya 37)

8. Burkina Faso (duniani nafasi ya 39)

9. Tunisia (duniani nafasi ya 56)

10. Afrika Kusini (duniani nafasi ya 58)