NRM: Museveni kuwania urais - 2011

Image caption Museveni Kuwania Urais Uganda

Baada ya miaka 24 madarakani Chama tawala nchini Uganda kimemteua bila kupingwa rais Yoweri Kaguta Museveni kama mgombea wake wa urais mwaka ujao 2011.

Uteuzi wa Museveni uliafikiwa kwenye kongamano la kitaifa la wajumbe wa chama cha National Resistance Movement,{NRM} mjini Kampala.

Lakini kongamano hilo lililokuwa la kuwachagua viongozi wa chama hicho, na ambalo limekuwa likiendelea usiku kucha limekumbwa na vurugu, huku baadhi ya vijana walionuia kuwania nyadhifa kadhaa wakilalamika kuwa wazee wana ng'ang'ania madarakani na kujitengea uteuzi biloa kuwazingatia wao.

Museveni

Rais Yoweri Kaguta Museveni alichukua hatamu za uongozi wa Uganda mnamo mwaka wa 86 wakati ambapo jeshi la waasi wa National Resistance Army lilipopindua serikali na kumtawaza kuwa rais. Baada ya kuwa uongozini kwa miaka 10, Museveni alichaguliwa kwa mara ya kwanza kuwa rais katika uchaguzi wa kitaifa mwaka wa 96.

lakini hata baada ya hapo vyama vya kisiasa vilikuwa vimezuiwa sana, na katikam waka wa 2000 wapiga kura wa Uganda wakakataa kuidhinisha mfumo wa vyama vingi. mwaka uliopita 2001, Museveni ambaye sasa alikuwa ametawala kwa miaka 15 aliwania tena urais. Katika uchaguzi huo uliokumbwa na mizozo, Museveni alimshinda mpinzani wake mkuu na mkuruba wake wa zamani Dr. Kizza Besigye ambaye alikuwa kibara wa chama cha upinzani FDC.

Katiba ya nchi

Kwa mujibu wa katiba ya Uganda, hiyo ilipaswa kuwa mara ya mwisho kwa Museveni kuwania wadhifa wa urais. lakini mnamo Juni 2005 bunge la Uganda lilipiga kura kufutilia mbali mihula ya rais na hivyo kumruhusu Museveni kuwania tena na tena wadhifa huo. Bila kuchelewa Februari mwakia uliofuta, 2006, Yoweri Museveni akawania tena katika kinyanganyiro cha Urais mpinzani wake mkuu akiwa yule yule Kizza Besigye.

Licha ya hayo yote Museveni alijishindia miaka mingine mitano madarakani. na sasa baada ya kuongoza kwa miaka 24 yuko tayari kuwakabili wapinzani wake katika uchaguzi wa mwaka ujao mkuu kati yao akiwa Kizza Besigye, kiongozi wa chama cha FDC.