Titus Bramble atuhumiwa kumbaka mwanamke

Titus Bramble
Image caption Titus Bramble

Mlinzi wa Sunderland Titus Bramble, amekamatwa baada ya mwanamke kubakwa kwenye hoteli moja mjini Newcastle.

Mchezaji huyo wa Ligi Kuu ya England amekamatwa pamoja na mtu mwengine katika hoteli ya Vermont mapema siku ya Jumatano na wanahojiwa na polisi.

Bramble mwenye umri wa miaka 29 amekamatwa kwa kushukiwa amebaka baada ya polisi kupigiwa simu na mwanamke mmoja.

Klabu ya Sunderland hadi sasa haijazungumza lolote kuhusiana na tuhuma hizo. Bramble alijiunga na klabu hiyo akitokea Wigan msimu huu.

Msemaji wa kituo cha polisi cha Northumbria, amesema wanaume wawili, wakiwa na umri wa miaka 29 na 30 wamekamatwa wakituhumiwa kubaka mwanamke.

Bramble pia aliwahi kuichezea New Castle na Ipswich.