Red Cross: 1B wanaishi maisha duni

Image caption nyumba za mabanda

Shirika la kimataifa la msalaba mwekundu linasema zaidi ya watu bilioni moja katika nchi zinazoendelea wanakabiliwa na tisho la maafa kwa sababu wanaishi kwenye maeneo duni yasiyo na huduma za dharura.

Utafiti unasema katika maeneo mengi ya Afrika,Asia na Amerika kusini zimeshindwa kukabiliana na ukuaji haraka wa miji.

Aidha ripoti hiyo imeonya kuwa tisho la maafa litaongezeka kwasababu ya mabadiliko ya hali ya hewa.

Ripoti hiyo imeangazia janga la tetemeko la ardhi la Haiti kama mfano wa namna maafa yanavyoweza kuyakumba maeneo ya mijini.