Caf yapata katibu mkuu mpya

Image caption Hicham el Amrani

Hicham el Amrani wa Morocco ameteuliwa katibu mkuu wa muda wa shirikisho la soka barani Afrika, Caf.

Uteuzi huo ulithibitishwa baada ya mkutano wa kamati ya utendaji ya Caf mjini Cairo, Misri, siku ya Alhamis.

Kijana huyo mwenye miaka 31 anachukua nafasi ya Mustapha Fahmy anayeondoka Caf kujiunga na Fifa kama mkurugenzi wa mashindano.

Uteuzi wa Amrani unaanza rasmi tarehe 1 Oktoba, na kupanda haraka kwa mtu huyo aliyejiunga na Caf mwaka 2009.

Aliacha kazi yake kama meneja masoko wa shirikisho la soka barani Asia ili kuwa katibu mkuu msaidizi wa Caf, ambaye alifanya kazi kwa ukaribu na Fahmy.

Rais wa Caf Issa Hayatou alimsifia Fahmy aliyekaa kwenye nafasi hiyo kama mkurugenzi mkuu wa chombo hicho.

Hayatou alimwambia Fahmy ambaye ni raia wa Misri, "Hapa ni kwako daima."

Fahmy amabye alikuwa katika hisia kali alimwaga machozi na kuzungumzia jinsi ilivyo "vigumu" kwake kuondoka kwenye shirikisho hilo.

Alisema "ataendelea kuwa mfanyakazi mwaminifu wa soka ya Afrika" wakati akifanya kazi na Fifa.