UN: Mpango mpya wa kuwanusuru wanawake.

Image caption Wanawake Kukombolewa

Umoja a Mataifa umezindua mpango mpya unaolenga kunusuru maisha ya wanawake na watoto milioni kumi na sita katika nchi zinazoendelea kwa kipindi cha miaka mitano ijayo.

Bwana Ban katika maeneo mengi duniani , bado wanawake hawajanufaika na faida za kuwawezesha kujifungua salama zaidi kwa zaidi ya miaka mia moja.

Amesema mamilioni ya watoto wanaendelea kufariki dunia kutokana na utapia mlo na magonjwa mengine ambayo yanaweza kutibiwa, suala ambalo amesema halikubaliki.