Arsenal, Chelsea zadunda

Arsenal ikicheza nyumbani imezabwa mabao 3-2 na West Brom.

Image caption Peter Odemwingie

Peter Odemwingie wa West Brom ndiye aliyeandika bao la kwanza dhidi ya Arsenal katika dakika ya 50, bao la pili likifungwa na Gonzalo Jara dakika mbili baadaye. Bao la tatu la WBA liliwekwa kimiani na Jerome Thomas katika dakika 72. Arsenal walicharuka na Samir Nasri kufunga bao la kwanza katika dakika ya 74, na la pili dakika ya 90.

Mapema, Chelsea nayo ilinyukwa bao 1-0 na Manchester City kwenye mchezo uliochezwa kwenye uwanja wa City of Manchester. Nahodha wa City Carlos Tevez ndiye aliandika bao hilo pekee la ushindi.

Liverpool nayo ililazimika kupigana kuime kuondoa aibu ya kufungwa nyumbani, baada ya kutoka sare ya 2-2 na Sunderland. Liverpool ndio iliazna kufunga kupitia mchezaji wake Dirk Kuyt katika dakika ya tano tu ya mchezo.

Darren Bant alisawazisha bao hilo kwa mkwaju wa penati dakika ya 25. Bent tena aliandika bao la pili muda mfupi baada ya mapumziko. Hata hivyo Liverpool walilazimika kucheza kufa na kupona, na nahodha Steven Gerrard lisawazisha goli hilo katika dakika ya 64.

Katika michezo mingine, Birmingham City ilitoka sare ya 0-0 na Wigan, Blackpool kunyukwa mabao 2-1 na Blackburn Rovers, Everton nayo kutoka sare ya 0-0 na Fulham, huku West ham ikiichapa Tottenham kwa 1-0.