Mashauriano: Korea Kusini na Kaskazini

Image caption Korea kusini na kaskazini zajadiliana

Wizara ya ulinzi ya Korea kusini imeanza mashauriano na Korea Kaskazini, ikiwa ni mazungumzo ya kwanza katika kipindi cha miaka miwili.

Uhusiano kati ya mataifa hayo mawili ulivunjika mwezi Machi baada ya Korea kusini kuishutumu Korea Kaskazini kwa kuzamisha manoari yake,shutuma ambayo Korea Kaskazini imekanusha.

Mapema wiki hii Korea ya Kaskazini iliambia baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kuwa itaendelea na mipango yake ya kujiimarisha kwa nguvu za kinuklia na wala haitasitisha miradi yake almuradi ndege za Marekani zinashika doria katika pwani zake.