Nigeria: Miaka 50 ya Uhuru

Image caption Miaka hamsini ya Uhuru wa Nigeria

Nigeria inajiandaa kwa sherehe ya kuadhimisha miaka hamsini ya uhuru kutoka kwa Uingereza, kwa maandamano katika miji yote nchini humo.

Mwandishi wa BBC nchini humo anasema kuwa maadhimisho hayo yamezua mjadala wa kimataifa juu ya taifa hilo lenye zaidi ya jamii mia mbili zinazoishi katika muungano usio thabiti.

Bado nchi hiyo inauguza historia ya majaribio ya mapinduzi na mapigano ya kikabila na kidini. Hata hivyo kiongozi wa zamani wa jeshi Yakubu Gowon ameambia BBC kuwa licha ya hayo matatizo yote nchi hiyo imeendelea mbele.