Perves Musharraf azindua chama kipya

Image caption Pervez Musharraf

Aliyekuwa rais wa Pakistan General Pervez Musharraf hii leo anazindua chama kipya cha kisiasa mjini London.

Aliambia BBC kuwa serikali ya Islamabad imeshindwa kuimarisha uchumi wa nchi na kutekeleza wajibu wake muhimu wa kuongoza serikali thabiti.

Amesema kuwa kwa sasa wananchi wa Pakistan wanategemea jeshi kuwarejeshea uogozi bora na kuwatatulia matatizo ya nchi yao.

Alionya pia kuwa ni muhimu kuunda demokrasia ya Pakistan kwa malengo ya Wapakistani wenyewe na sio shinikizo za mataifa ya magharibi.

Musharraff Alisema kuwa anazindua chama chake mjini London kwa hofu ya kuuwawa akirejea Pakistan.