Marekani yashutumu mashambulio - Nigeria

Image caption Bomu mjini Abuja

Marekani imesema kuwa mashambulio ya bomu ya hapo jana nchini Nigeria inaashiria umuhimu wa kufanyika uchaguzi wa mwaka ujao.

Msemaji wa idara ya serikali P.J Crowley Marekani imeshutumu vikali mashambulio hayo yaliyotokea katika mji mkuu Abuja wakati wa sherehe za kuadhimisha miaka hamsini ya Uhuru wa Nigeria .

Takriban watu wanane wameripotiwa kuuawa katika mashambulio hayo.

Kundi la waasi la MEND linalopigania umiliki wa kiasi kikubwa cha mafuta ya Nigeria limedai kuhusika na shambulio hilo.