Congo imekuwa "Mj imkuu wa ubakaji"

Image caption Margot Wallstrom

Mjumbe maalum wa Umoja wa mataifa juu ya dhuluma za kimapenzi katika mapigano ametoa wito wa hatua kuchukuliwa kusitisha utumiaji wa ubakaji kama silaha ya vita katika Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo.

Margot Wallstrom aliyasema haya alipozuru mji wa walikale ambapo mnamo mwezi Agosti kuliripotiwa visa vya ubakaji wa wanawake, watoto wa kike na hata wa kiume, vilivyofanywa na wanajeshi katika kipindi cha siku nne.

Bi Wallstrom pia ametoa wito wa kikosi cha kulinda amani nchini humo kuchukua hatua zaidi kuwalinda raia katika eneo hilo.

Alitaja Congo kuwa mji mkuu wa ubakaji dunia nzima.