Odemwingie mchezaji bora Septemba

Meneja wa West Brom Robert Di Matteo amechaguliwa meneja bora wa Ligi Kuu ya England kwa mwezi wa Septemba.

West Brom wamefanikiwa kuzoa pointi saba katika mechi zao tatu zilizopita, ikiwemo dhidi ya Manchester City na Arsenal na wanashikilia nafasi ya sita ya msimamo wa ligi.

Na mshambuliaji Peter Odemwingie amechaguliwa mchezaji bora kwa mwezi wa Septemba.

Image caption Peter Odemwingie

Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Nigeria, aliyejiunga na West Brom akitokea klabu ya Lokomotiv Moscow mwezi wa Agosti, amekuwa akifanya vizuri mzimu huu na amefunga mabao matatu katika mechi tano alizocheza.