Okah asema hakuhusika na mashambulizi Nigeria

Henry Okah
Image caption Henry Okah

Aliyekuwa kiongozi wa waasi nchini Nigeria Henry Okah amekanusha kuhusika katika mashambulizi ya mabomu ya hivi karibuni katika mji mkuu wa Nigeria, Abuja.

Akizungumza katika mahakama moja nchini Afrika Kusini, alisema kuwa hajawahi kukutana na watu tisa waliotiwa mbaroni nchini Nigeria baada ya mashambulizi hayo.

Pia alikanusha kuendelea na uongozi wa shughuli za kundi la waasi la Nigeria linalofahamika (MEND), ambalo lilisema lilihusika na mashambulizi hayo.

Waendesha mashtaka walimshtumu Bw Okah, ambaye anaishi Afrika Kusini, kwa kupanga mashambulizi hayo ya mabomu.

Mashambulizi hayo yaliwauwa watu kumi na wawili wakati Nigeria ikisherehekea miaka hamsini ya uhuru wake.