Pele atimiza umri wa miaka 70

Siku ya Jumamosi tarehe 23 mwezi wa Oktoba, msakata kandanda wa zamani bora zaidi dunia Pele alitimiza umri wa miaka 70.

Image caption Pele atimiza miaka 70

Pele ambaye jina lake kamili ni Edson Arantes do Nascimento alizaliwa huko Tres Coracoes jimbo la Minas Gerais, alianza kuichezea timu yake ya taifa ya Brazil akiwa na umri wa miaka 17 na kuisaidia nchi yake kushinda Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza mwaka 1958.

Pia alikuwemo katika kikosi kilichotetea taji hilo mwaka 1962 na baadae akawemo katika kikosi bora zaidi cha Brazil kilichoshinda Kombe hilo 1970 nchini Mexico na kuweka rekodi ya Brazil kushinda Kombe la Dunia mara tatu.