Khumalo:Nitajitahidi nipewe nafasi ya kwanza

Bongani Khumalo
Image caption Bongani Khumalo

Mchezaji wa Afrika kusini aliyesajiliwa na klabu ya Tottenham,Bongani Khumalo ameahidi kuwa ataania kuchezea kikosi cha kwanza.Hii ni baada ya kuthibitishwa kuhama kwake kwa pauni za Uingereza milioni £1.5.

Licha ya kuwa na ushindani mkali kutoka kwa wachezaji wanaocheza katika safu ya ulinzi kama vile William Gallas, Ledley King na Sebastian Bassong.

Khumalo anaamini anaweza kujipatia nafasi kwenye kikosi cha kwanza cha wachezaji kumi na moja.

Bongani Khumalo anatarajiwa kwenda Tottenham mwezi wa januari iwapo atapa kibali cha kufanya kazi Uingereza.