Meya wa Nairobi apewa dhamana

Meya wa jiji la Nairobi amekanusha madai yanayomkabili ya kuhusika na njama za kufilisi baraza la jiji la Nairobi zaidi ya dola milioni tatu nukta tano.

Image caption Nairobi

Geoffrey Majiwa aliachiliwa kwa dhamana huku akisubiri siku ya kusikilizwa kwa kesi dhidi yake.

Majiwa ndie afisa mmwandamizi kushtakiwa kwa kashfa hiyo ambapo inadaiwa ardhi iliokusudiwa kutumiwa kwa makaburi ililipiwa mara kumi zaidi ya gharama yake halisi.

Kwa mujibu wa katiba mpya ya Kenya iliyoidhinishwa na Wakenya miezi miwili iliyopita, afisa yeyote wa umma atakayeshtakiwa mahakamani kwa makosa ya ufisadi, atalazimika kujiuzulu au kuondolewa madarakani kwa lazima.