Mechi za Carling:Newcastle 0- 4 Arsenal

Arsenal
Image caption Arsenal

Katika mechi za jana usiku za kombe la carling Arsenal iliifunga New castle magoli manne sifuri.

Baada ya kipindi cha kwanza arsenal ilikuwa na goli moja tu,lakini kipindi cha pili Theo Walcott aliingiza mawili naye Nicklas bendtner akaingiza bao moja kukamilisha idadi ya magoli manne.

Katika mechi zengine za kombe la carling zilochezwa Jumatano usiku Aston villa waliifunga Burnley mabao mawili kwa moja huku West ham wakiwakomalia stoke city kwa kujipatia mabao matatu kwa moja.