Tsunami Indonesia:Waliokufa sasa ni 282

Juhudi za uokoaji Indonesia
Image caption Juhudi za uokoaji Indonesia

Idadi ya waliofariki dunia kufwatia tsunami katika visiwa vya nchini Indonesia imeongezeka hadi 282,maafisa wamesema.

Vikosi vya uokoaji katika visiwa vya Mentawai wanasema mamia ya watu bado hawajulikani walipo,siku mbili baada tetemeko la ardhi kusababisha tsunami magharibi mwa Sumatra.

Maafisa wanasema kulikuwa na matatizo katika mtambo uliotengenezwa kwa lengo la kutoa tahadhari kwa wakaazi juu ya kuzidi kwa mawimbi.

Rais wa Indonesia amekatiza ziara yake ya nchini Vietnam ili aweze kutembelea visiwa hivyo pamoja na kusimamia shughuli za uokozi.

Rais Susilo Bambang Yudhoyono anatarajiwa kuzuru eneo hilo siku ya alhamisi kutathmini juhudi za misaada.

Pia ataelezwa kuhusu uokoaji katika eneo la Java, ambapo mlipuko wa volcano umesababisha maafa.