Mkuu wa soka Zimbabwe atimuliwa

Henrietta Rushwaya
Image caption Henrietta Rushwaya

Afisa mwandamizi wa shirikisho la soka la Zimbabwe (ZIFA) Henrietta Rushwaya amefutwa kazi.

Maafisa wa Zifa wametangaza kuwa kufutwa kwa Rushwaya siku ya Jumanne,ni kutokana na "usimamizi mbaya".

Lakini madai ya kupanga mechi dhidi yake wakati wa timu ya taifa ilipofanya ziara ya bara Asia Desemba iliopita yameondolewa huku uchunguzi zaidi ukifanywa.

Katika kashfa hio inadaiwa pia wachezaji maarufu,makocha na viongozi wengine walihusika.

Image caption Mashabik wakati wa mechi kati ya Bafanabafana na Zimbabwe

Katika taarifa zao,wachezaji wa Zimbabwe na maafisa wamesema kuwa walilipwa kati ya $500 na $1,500 ili wapange matokeo kwa ajili ya kamari huko Thailand na Malaysia.

Wanakabiliwa na marufuku ya maisha,jambo linalotishia mustakabali wa wachezaji wa kulipwa katika taifa hilo la kusini mwa Afrika.