Drogba azindua kampeni uchaguzi wa haki

Mwanasoka nyota Didier Drogba leo amezindua kampeni ya kuweka bayana suala la demokrasia na uchaguzi wa wazi sehemu mbalimbali duniani kuwa ni chombo muhimu kwa kuziondoa nchi masikini duniani katika lindi hilo la umasikini.

Image caption Didier Drogba

Drogba, aliyeongoza nchi yake ya Ivory Coast katika fainali za Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza mwaka 2006, amezindua bango lililokuwa na ujumbe usemao “Teremka uwanjani, na umwe mchezaji. Jisajili. Piga Kura. Usikilizwe.”“Ili maendeleo yapatikane, hatuna budi kuhakikisha uchaguzi wa haki na uwazi", amesema Drogbas,” .Ameongeza: “Ninaamini utawala bora unaweza kusaidia nchi kuondokana na umasikini, ikiwa tu wasimamizi wa uchaguzi na wanasiasa watatimiza jukumu lao.”Ikiwa nchi nyingi za Afrika zikikabiliwa na uchaguzi katika miaka michache ijayo, ambako nchi zinazoendelea na masikini zipo, Drogba amesema: “Matumaini yangu ni kusaidia kuchangia katika suala la demokrasia barani Afrika. Ndio maana ninahubiri ukweli na uchaguzi ulio huru, ndio njia pekee kwa Afrika kusonga mbele.”Bango hilo alilozindua lina picha ya Drogba akijiandaa kupiga mkwaju wa penalti, akiwa amevalia fulana ya timu ya taifa ya Ivory Coast yenye rangi ya machungwa. Bango hilo litazinduliwa mjini Kinshasa, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, ambako uchaguzi aina nane umepangwa kufanyika katika miaka mitatu ijayo, ikiwa ni wa urais, wabunge, majimbo na kiwango cha manispaa.