EU kudhibiti msukosuko wa kifedha

Euro
Image caption Euro

Viongozi wa muungano wa Ulaya wamekubaliana kuhusu mpango wa kudumu utakaolinda muungano huo kutoka na msukosuko wa kifedha.

Pia wamekubaliana kuwa na mbinu moja itakayokokabiliana na nchi yeyote itakayotishia udhibiti wa sarafu moja kama Ugiriki mapema mwaka huu. Viongozi hao wamekubaliana kuimarisha udhibiti katika nchi zinazotumia sarafu ya euro. Hatua hiyo itauwezesha muungano huo kuchunguza bajeti za nchi wanachama,kutoa ushauri kuhusu mipango ya kibiashara ambayo huenda ikaleta hasara,kutoza faini nchi zinazoomba mikopo na kutumia fedha nyingi.

Image caption Maandamano ya Ugiriki mapema mwaka huu

Mpango huo utarahisisha utekelezaji wa hatua kama hizo.

Ni mpango unaonuiwa kulazimisha nchi wanachama, kusuluhisha matatizo yao ya kifedha kabla matatizo hayo kuanza kutishia nchi zingine zinamazotumia sarafu ya euro.

Pia utakuwa na mfuko wa dharura utakaochukua nafasi ya ule wa muda uliowekwa ili kukwamua nchi ya Ugiriki.

Lakini kwa hilo kufanyika Ujerumani inasisitiza kuwa ni lazima mkataba wa Lisbon ufanyiwe marekebisho.

Rais wa baraza la Muungano wa Ulaya Herman Van Rumpey, amepewa kazi ya kuangalia jinsi hilo litakavyowezekana bila kubadilisha mkataba wa Lisbon katika nchi zote 27.