Misaada yawasili Indonesia

Mkaazi wa kisiwa cha Mentawai magahribi mwa Sumatra
Image caption Mkaazi wa kisiwa cha Mentawai magahribi mwa Sumatra

Misaada imeendelea kuwafikia wale waliokumbwa na maafa Indonesia baada ya meli tatu kufika katika kisiwa kilichoharibiwa zaidi na tsunami.

Vikosi vya uokoaji sasa wanajitahidi kusaidia watu katika kisiwa cha Pagai Kaskazini magharibi mwa Sumatra.

Inafahamika kuwa zaidi ya watu 340 wamefariki dunia.Mamia bado hawajulikani walipo.

Image caption Rais wa Indonesia

Rais wa Indonesia ametembelea visiwa hivyo.

Rais Susilo Bambang Yudhoyono alikatiza safari yake huko Vietnam ili kusimamia shughuli ya uokoaji,na alisafiri kwa helikopta ambayo ilikuwa imebeba vyakula na bidhaa zengine muhimu.

Huko alikutana na wale walionusurika pamoja na viongozi wa eneo hilo.

Ameahidi kuwa serikali itasaidia utawala wa Sumatra Magharibi kujenga nyumba za muda, vituo vya afya na shule, msemaji wake alisema.

Msaada huo umefika huku Indonesia ikikabiliana na maafa mengine yaliyoletwa na mlipuko wa mlima Merapi katikati mwa Java.

Zaidi ya 30 waliuawa.