Angola ichunguze madai ya ubakaji

Mmoja wa wanawake waliobakwa Congo
Image caption Mmoja wa wanawake waliobakwa Congo

Marekani imetoa wito kwa Angola kuchunguza madai ya wanawake ambao waliorudisha jamhuri ya kidemokrasi ya Congo kutoka Angola kubakwa.

Marekani inasema kuwa nchi zote mbili zina wajibu wa kulinda wanawaeke na watoto.

Msemaji wa mambo ya nje wa Marekani, Philip Crowley, amesema lazima nchi zote mbili ziangalie suala la raia kuhama kutoka nchi moja hadi nyengine katika mpaka wao.

Mwaka 2004, Angola ilizindua kampeini ilosababisha kufukuzwa kwa zaidi wahamiaji haramua laki nne.

Wengi wao walikuwa raia wa Congo na walifukizwa kutoka maeneo ya kuchimba madini.

Serikali ya Congo nayo ikalipiza kisasi kwa kuwafukuza raia wa Angola waliokuwa wakiishi karibu na maeneo ya mpakani.