Obama na Mbeki kura ya maoni kuendelea Sudan

Raia wa Sudan Kusini
Image caption Raia wa Sudan Kusini

Rais Barack Obama na rais wa zamani wa Afrika Kusini, Thabo Mbeki, wametoa wito wa kufanyika kura ya maamuzi kama ilivyokuwa imepangwa.

Sudan inatarajiwa kuandaa uchaguzi mbili tarehe 9 mwezi Januari mwaka ujao. Moja ni kuhusu uhuru wa eneo la Sudan Kusini na nyingine kuhusu mustakabali wa jimbo la Abiyei lenye utajiri mkubwa wa mafuta, eneo linalozozaniwa na serikali za Sudan Kusini na Kaskazini.

Katika mazungumzo ya simu Rais Obama na bwana Mbeki ambaye anaongoza jopo maalum la Umoja wa Afrika wamekubaliana kuhusu umuhimu wa kutafuta msaada kutoka jamii ya kimataifa katika maandalizi ya kura hiyo hapo mwakani.

Viongozi wa eneo la Sudan Kusini wameilaumu chama tawala katika eneo la Kaskini National Congress Party NCP, kinachoongozwa na rais Omar Al Bashir, kwa kuhujumu maandalizi ya Kura hiyo ya Maoni.