Uchaguzi mkuu kuandaliwa kesho Tanzania

Raia wa Tanzania wanajiandaa kwa uchaguzi mkuu ambao unatarajiwa kuandaliwa hapo kesho.

Image caption Wafuasi wa chama cha CCM

Vyama vya kisiasa vinatarajiwa kukamilisha kampeini zao hii leo.

Wafuasi wa rais wa nchi hiyo, Jakaya Kikwete wanatarajiwa kufika jijini Dar es Salaam, kuhudhuria mkutano wa mwisho wa kampeini,wa chama tawala cha CCM.

Kuna ushindani mkali katika kinyanganyiro cha kuwania kiti cha urais.

Miongoni mwa watu wanaowania kiti hicho ni pamoja na rais wa sasa Jakaya Kikwete ambaye alizoa asilimia 85 ya kura zote zilizopigwa wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2005.

Image caption Rais Jakaya Kikwete

Wakosoaji wa Rais Kikwete wanasema ameshindwa kukabiliana na ufisadi na kuhakikisha kuwa rasilimali ya nchi inawafikia raia wa Kawaida.

Rais Kikwete atapamabana wapinzani wengine akiwemo Willibrod Slaa ambaye ameahaidi kupambana na ufisadi na kuanzisha huduma za afya na elimu bila malipo nchini humo endapo atachaguliwa kuongoza taifa hilo.

Mwingine ni Ibrahim Lipumba ambaye amehaidi kubuni serikali ya muungano wa kitaifa ili kutatua matatizo ya taifa hilo ikiwa atashinda uchaguzi huo.

Wapiga kura milioni 19.6 wanatarajiwa kushiriki katika zoezi hilo.