Watu 30 wauawa kanisani Baghdad Iraq

Maafisa wa ulinzi nchini Iraq wamesema zaidi ya watu 30 wameuawa na wengine hamsini kujeruhiwa kwenye mapigano makali kati ya maafisa wa kijeshi na waasi waliowateka waumini wa kanisa moja la Katoliki katika mji mkuu Baghdad.

Image caption Kijana aliyeokolewa kanisani Baghdab

Wapiganaji hao walivamia kanisa hilo wakati wa ibada ya jioni siku ya Jumapili na kuwateka nyara waumini hao.

Taarifa zinasema kulikuwa na zaidi ya waumini mia moja na ishirini ndani ya kanisa hilo.

Wanajeshi walizingira kanisa hilo kabla ya kulivamia huku ndege za kijeshi zikitanda angani zikipiga doria.

Shambulio hilo lilianza wakati watu hao waliojihami kwa bunduki ambao wanaaminika ni wapiganaji wa al Qaeda walipojaribu kushambulia soko la hisa la Baghdad.