Mtuhumiwa Guantanamo ahukumiwa miaka 40

Mahakama ya kijeshi katika gereza la Guantanamo Bay imemhukumu kijana moja mpiganaji wa kundi la kigaidi la Al Qaeda Omar Khadr, kifungo cha miaka arobaini jela baada ya kupatikana na makosa ya mauaji na ugaidi.

Image caption Gereza la Guantanamo

Lakini kutokana na jinsi alivyojitetea, Khadr atatumikia kifungo cha miaka minane pekee.

Omar Khadr alikamatwa nchini Afghanistan mwaka wa 2002 akiwa na umri wa miaka kumi na mitano, wakati wa mapigano makali ya risasi kati ya wanajeshi wa Marekani na wapiganaji wa Kiislamu. Mshukiwa huyo alikiri mashtaka dhidi yake yakiwemo mauaji ya mwanajeshi mmoja.

Marekani imesema mshukiwa huyo atarejeshwa nyumbani kwao nchini Canada baada ya kutumikia kifungo cha mwaka mmoja gerezani nchini humo.