Kura zinahesabiwa nchini Tanzania

Wafuasi wa CCM
Image caption Wafuasi wa CCM

Shughuli ya kuhesabu kura inaendelea nchini Tanzania siku moja baada ya uchaguzi mkuu uliokuwa na msisimuko mkubwa kuwahi kushuhudiwa tangu kuanzishwa siasa za vyama vingi nchini humo miaka ya 1990.

Matokeo ya mwanzo yanatarajiwa siku ya Jumatano.

Rais wa sasa Jakaya Kikwete amesema anatarajia kutetea kiti hicho cha Urais.

Kikwete alikabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa Willibrod Sla ambaye alitumia muda mwingi wakati wa kampeini kupinga ufisadi.

Image caption Wafuasi wa chama cha CUF

Chama tawala cha Mapinduzi CCM, ambacho kimekuwa madarakani tangu nchi hiyo ilipojinyakulia uhuru, ilikabiliwa na upinzani mkali kutoka vyama kadhaa vya kisiasa, kufuatia kushuka kwa umaarufu wa serikali kutokana na madai ya ufisadi.

Kura kadhaa za maoni zimeonesha Rais Kikwete huenda akashinda muhula mwingine kuwa Rais wa nchi hiyo.

Hata hivyo kura nyingine ya maoni ilionyesha mpinzani wa Rais Kikwete, Wilbord Slaa wa chama cha CHADEMA alikuwa akiongoza japo kwa kiasi kidogo sana.