Spurs yawika, Man United yaua

Meneja wa Tottenham Harry Redknapp amesifia usakataji wa soka wa Gareth Bale katika mechi ya ligi ya mabingwa wa Ulaya walipowalaza mabingwa watetezi Inter Milan mabao 3-1.

Image caption Tottenham yaadhiri Inter Milan

Katika mechi ya kwanza iliyochezwa San Siro mwezi wa Oktoba, Bale alifunga mabao matatu peke yake na mechi ya marudiano siku ya Jumanne alisaidia kutoa pasi za krosi zilizozaa mabao.

Redknapp amemuelezea winga huyo wa kushoto: "Anaweza kutoa pasi za krosi,, mguu wake wa kushoto ni hatari anapokimbia, anaweza kupiga mashuti makali, anapiga chenga, kupigwa vichwa ana kila kitu.

Kwa ushindi huo Tottenhama wanaogoza kundi lao la A wakiwa na pointi saba sawa na Inter Milan, lakini wanatofautiana mabao.

Nayo Manchester United ushindi wake wa mabao 3-0 dhidi ya Bursaspor umekuja huku wakipata balaa la kuumia winga wake wa kutumainiwa Nani na kiungo Darren Fletcher .

Nani litoka uwanjani akichechemea akilalamika matatizo ya nyonga na kuna kila dalili hataweza kucheza mchezo wa Jumamosi wa Ligi Kuu ya England dhidi ya Wolves, huku Fletcher, aliyefunga bao la kwanza ameumia kifundo cha mguu. Kuna uwezekano Fletcher naye asiweze kucheza Jumamosi.

Manchester wanaongoza katika kundi C wakiwa wamezoa pointi 10 hadi sasa wakifuatiwa na Valencia wenye pointi 7 ambao waliwachabanga Rangers ya Scotland mabao 3-0.

Ilikuwa ni mara ya kwanza kwa Rangers kufungwa katika mashindano yoyote msimu huu, hali inayowaweka katika nafasi ya tatu ya kundi hilo la C wakiwa na pinti tano tu.

Matokeo ya mechi nyingine za Jumanne za Ubingwa wa Ulaya:

Benfica 4-3 Lyon

FC Copenhagen 1-1 Brcelona

Hapoel Tel-Aviv 0-0 Schalke 04

Rubin Kazan 0-0 Panathinaikos

Tottenham 3-1 Inter Milan

Werder Bremen 0-2 FC Twente