Watu 3 washtakiwa kwa kufadhili Al Shabaab

Wapiganaji wa Al Shabaab nchini Somalia
Image caption Wapiganaji wa Al Shabaab nchini Somalia

Kwa mara ya pili wiki hii viongozi wa mashtaka nchini Marekani, wamewafunguliwa mashtaka raia wake kwa kufadhili kundi la kigaidi ya Al Shabaab nchini Somalia.

Dereva mmoja wa taxi, Mohamud Abdi Yusuf na mfanyakazi mmoja wa kampuni ya kutuma pesa mjini Minneapollis, Abdi Madhi Hussein wameshtakiwa kwa kutoa maelfu ya madola kwa kundi hilo la Al Shabaab.

Mshukiwa wa tatu, Dunae Mohamed Diriye pia alifunguliwa mashtaka bila ya kuwepo mahakamani.

Mshukiwa huyo anashukiwa amejificha nchiniSomalia au Kenya.

Hapo jana raia watatu wa Somalia wanaoishi katika jimbo la Carlifonia walifunguliwa mashtaka ya kufadhili kundi hilo la Al Shabaab.