Wafanyakazi BBC warejea kazini

Waandishi wa habari wa BBC wamekuwa wakirejea kazini baada ya mgomo wao wa saa 48.

Image caption Wafanyakazi wa BBC walipogoma

Wajumbe wa Chama cha Waandishi wa Habari cha taifa walikuwa wakipinga marekebisho ya malipo ya uzeeni ya wafanyakazi.

Baadhi ya vipindi vya BBC viliathirika kutokana na mgomo huo.

Chama wa waandishi wa habari kinapanga mgomo mwingine wa saa 48, unaotarajiwa kuanza tarehe 15 mwezi huu Novemba.