Uchaguzi wafanyika Burma baada ya miaka 20

Viongozi wa kijeshi wa Burma
Image caption Viongozi wa kijeshi wa Burma

Burma inafanya uchaguzi wake mkuu wa kwanza katika kipindi cha miaka 20 hii leo.

Wagombea huru wamekabiliwa na vikwazo katika utaratibu wa kujiandikisha na kufanya kampeni, huku kukiwa na shutma kuwa jeshi linataka kuendelea kutawala likitumia vyama ambavyo ni vibaraka vyake.

Waandishi wa habari wa kigeni na wakaguzi wamepigwa marufuku kurepoti au kusimamia uchaguzi huo.

Chama kikuu cha upinzani, National League for Democracy, kinacho-ongozwa na mshindi wa tuzo ya Nobel, Aung San Suu Kyi, kinasusia uchaguzi huo, lakini kundi lililoasi ndani ya chama hicho linashiriki.

Licha ya mataifa kadhaa ya magharibi kuhoji jinsi uchaguzi huo unavyoendeshwa, wadadizi wa mambo wanasema mabadiliko fulani yanayeweza kupatikana nchini humo kutokana na kura hiyo.