Genge la mihadarati lachachamaa Mexico

Watu wenye silaha kaskazini mwa Mexico wameweka vizuizi barabarani pamoja na mabango yenye maandishi ya vitisho, siku moja baada ya kiongozi mkuu wa genge la madawa ya kulevya kuuwawa ne jeshi katika mapambano.

Image caption Mapambano dhdi ya mihadarati Mexico

Wakaazi waliarifu kusikia milio mikubwa ya risasi baada ya vizuizi vya barabarani kuwekwa katika mji wa Reynosa, ngome kuu ya genge la Gulf, ambalo kiongozi wake Ezequiel Cardenas, kwa jina maarufu Tony Tormenta, alipigwa risasi na kuuwawa siku ya Ijumaa.

Katika miji mingine kwenye jimbo la Tamaulipas, genge jingine hasimu la Zetas liliweka mabango kusherehekea kifo cha Tormenta.