Askari polisi auwa watu 10 Kenya

Maafisa wa serikali ya Kenya wamesema askari polisi aliyehamaki amewapiga risasi na kuwauwa watu kumi.

Image caption Siakago eneo kulipotokea mauaji

Mkuu wa polisi wa mji wa Siakago, Marcus Ochole amesema maafisa wa polisi wanachunguza taarifa za mauaji hayo yaliyotokea usiku wa kuamkia Jumapili katika mji huo, kaskazini mashariki mwa Nairobi. Mwandishi habari katika eneo la hilo amesema askari polisi huyo alifyatua risasi holela katika baa tatu tofauti na kuuwa watu wawili katika baa mbili na wengine wanane katika baa ya tatu.

Taarifa zinasema mamia ya watu walifanya maandamano nje ya kituo cha polisi mjini humo.