Marekani yazungumza na Yemen kuisaidia

Waziri wa Ulinzi wa Marekani, Robert Gates, amesema Marekani inafanya mazungumzo na Yemen kuhusu namna ya kuisaidia kupambana na wanamgambo wa kundi la Al-Qaeda katika rasi ya Uarabuni.

Image caption Waziri wa Ulinzi wa Marekani, Robert Gates

Akizungumza wakati wa ziara yake nchini Australia, Bw Gates amesema msaada wowote mpya kutoka Marekani utazingatia zaidi mafunzo kwa jeshi la Yemen.

Wiki iliyopita, kundi la Al-Qaeda lenye makao yake nchini Yemen lilikiri kuhusika na vifurushi viwili vya mabomu vilivyopatikana hivi karibuni kwenye ndege za mizigo nchini Uingereza na Dubai.