Iran kutojili suala la nyuklia mkutanoni

Rais wa Iran, Mahmoud Ahmadinejad, amesema nchi yake haitajadili suala la nyuklia katika mkutano uliopendekezwa baadaye mwaka huu.

Image caption Rais wa Iran Mahmoud Ahmadinejad

Katika hutuba kupitia televisheni Ahmadinejad amesema Iran imeweka wazi mara kadhaa haiwezi kufanya mazungumzo kuhusu haki yake ya kuwa na miradi ya nyuklia.

Matamshi yake ni kinyume na yaliyotolewa na maafisa wa Iran waliosema nchi hiyo iko tayari kuhudhuria mkutano huo uliopangwa kufanyika nchini Uturuki na kuzijumuisha Marekani, Urusi , China, Ufaransa na Ujerumani.