Kipindupindu chawaua watu 540 Haiti

Madaktari katika mji mkuu wa Haiti, Port au Prince, wamesema mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu umetokea mjini humo ingawa hapajakuwa na thibitisho rasmi.

Image caption Kipindupindu chazidi Haiti

Zaidi ya watu 540 wamekufa kufuatia maradhi hayo na wengine takriban 8000 wanatibiwa hosipitalini.

Kuna wasiwasi maradhi hayo huenda yakasambaa kwa haraka katika kambi za mji wa Port-au-Prince zinazowasitiri waathiriwa wa tetemeko la ardhi lililotokea mwezi Januari mwaka huu.

Juhudi za kukabiliana na maambukizi ya ugonjwa huo zinavurugwa na mafuriko yaliyosababishwa na kimbunga cha Tomas kilichopiga Haiti mwishoni mwa juma.