Barack Obama awasili Indonesia

Rais wa Marekani Barack Obama amewasili nchini Indonesia ambako kuna idadi kubwa ya Waislamu duniani katika ziara yake barani Asia.

Image caption Rais Obama na mkewe wakiwasili Jakarta

Wakati wa ziara yake Rais Obama atatangaza makubaliano ya ushirikiano na kuitambua Indonesia kuwa mshirika wa karibu wa Marekani.

Pia anatarajiwa kuwasilisha ujumbe wa heshima kwa Waislamu.

Hii ni mara ya kwanza Rais Obama kuitembelea Indonesia tangu aingie madarakani. Aliishi nchini humo utotoni mwake.