Balotelli na Kocsielny kutumikia adhabu

Rufaa za klabu za Manchester City na Arsenal dhidi ya kadi nyekundu walizooneshwa wachezaji wao zimegonga mwamba.

Image caption Laurent Koscielny

Mlinzi wakati wa Arsenal Laurent Koscielny anatakiwa kutumikia adhabu ya kutocheza mechi mbili baada ya chama cha Soka cha England kutupilia mbali rufaa ya Arsenal iliyopinga adhabu hiyo wakati walipocheza na Newcastle.

Koscielny alitolewa nje kwa kadi nyekundu dakika za mwisho za mchezo baada ya kumzuia mshambuliaji wa Newcastle Nile Ranger siku Arsenal ilipofungwa bao 1-0.

Na kwa upande wa mshambuliaji wa pembeni wa Manchester City, Mario Balotelli, naye rufaa yake imetupwa na anatakiwa kutumikia adhabu ya kutocheza mechi tatu.

Balotelli alioneshwa kadi nyekundu wakati Manchester City walipowalaza West Browm mabao 2-0, baada ya kuonekana akimtandika teke Youssuf Mulumbu.

Kwa hiyo atakosa mechi dhidi ya Manchester United siku ya Jumatano, mechi na Birmingham siku ya Jumamosi na ile ya umapili ijayo watakapokutana na Fulham.